TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
1.0 Serikali inatarajia kuajiri Walimu 92 wa Shahada na 174 wa
Stashahada wa masomo ya Fizikia, Hisabati, Kilimo na Biashara kwa Shule
za Sekondari na Walimu 2,767 wa Cheti kwa Shule za Msingi.
2.0
Waombaji kwa shule za Sekondari wawe waliohitimu mafunzo ya Ualimu mwaka
2016 au kabla, na wale wa Shule za Msingi wawe waliohitimu mafunzo yao
mwaka 2014 au kabla.
3.0 Sifa za Waombaji:
3.1 Walimu wa Sekondari:
(i) Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu
(Bachelor of Education) yenye somo moja la kufundishia au zaidi au
Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo moja la kufundishia au zaidi
pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in
Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
Masomo ya kufundishia ni kati ya Fizikia, Hisabati, Kilimo au Biashara.
(ii) Stashahada ya Ualimu katika masomo yaliyoainishwa kwenye kipengele Na. 2.1 (i) hapo juu.
(iii) Cheti cha Kidato cha Sita
(iv) Cheti cha Kidato cha Nne
3.2 Walimu wa Shule za Msingi:
(i) Astashahada ya Ualimu iliyotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(ii) Cheti cha Kidato cha Nne (wenye cheti Kidato cha Sita watapewa kipaumbele).
4.0 Utaratibu wa Kutuma Maombi:
(a) Maombi yatumwe kupitia Posta kwa njia ya Rejesta (EMS). Juu ya
bahasha iandikwe kwa mkono "Maombi ya Kazi ya Ualimu - Sekondari au
Maombi ya Kazi ya Ualimu - Msingi".
(b) Mwombaji aambatishe nakala za Vyeti vilivyothibitishwa (Certified) na Mwanasheria pamoja na "Transcript".
NB: Barua za maombi zisiwasilishwe kwa mkono. Barua zitakazowasilishwa kwa mkono hazitapokelewa.
5.0 Masuala Mengine ya Kuzingatia:
(a) Mwombaji aandike majina yake yote matatu. Kama Vyeti vina majina
mawili, utaratibu wa kisheria wa kuongeza jina uzingatiwe.
(b) Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.
Mwisho wa kupokelewa maombi ni tarehe 31/08/2017.
Maombi yatumwe kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA