Dereva Daraja La II --Halmashauri Ya Wilaya Ya Chunya

Application Deadline: 04 Mar 2015
Dereva Daraja La II - (TGOS A) POSITION DESCRIPTION:
From Mwananchi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wialaya Chunya anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzia wenye sifa zinazotakiwa ili kujaza nafasi za kazi zifuatazo:-

Dereva Daraja La II - (TGOS A)
Sifa
Mwombaji awe na Elimu ya kidato cha (IV), mwenye Leseni daraja “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usioppungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, mwenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II

Kazi na Majukumu
(i) Kuendesha magari ya abiria na malori
(ii) Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitajika matengenezo
(iii) Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari; na
(iv) Kutunza na kuandika daftari la safari “Log - book kwa safari zote

MASHARTI KWA UJUMLA
(i) Mwombaji sharti awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45
(ii) Waombaji walio katika ajira wapitishe maombi kwa waajiri wao
(iii) Mwombaji aambatanishe picha 2 (Passport size) na nakala za vyeti katika barua ya maombi
(iv) Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04/03/2015
(v) Tarehe ya usaili kwa watakaokidhi vigezo itatangazwa baadae

APPLICATION INSTRUCTIONS:
Maombi yatumwe kwa:

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA
S.L.P 73
CHUNYA
Dereva Daraja La II --Halmashauri Ya Wilaya Ya Chunya Dereva Daraja La II --Halmashauri Ya Wilaya Ya Chunya Reviewed by ISSAH JUMA on Wednesday, February 18, 2015 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.