Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya, June 26 2016 huu hapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
  1. Arusha            Mrisho Mashaka Gambo
  2. Arumeru            Alexander Pastory Mnyeti
  3. Ngorongoro            Rashid Mfaume Taka
  4. Longido            Daniel Geofrey Chongolo
  5. Monduli            Idd Hassan Kimanta
  6. Karatu            Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
  1. Kinondoni           Ally Hapi
  2. Ilala           Sophia Mjema
  3. Temeke            Felix Jackson Lyaviva
  4. Kigamboni            Hashim Shaibu Mgandilwa
  5. Ubungo            Hamphrey Polepole
DODOMA
  1. Chamwino           Vumilia Justine Nyamoga
  2. Dodoma            Christina Solomon Mndeme
  3. Chemba            Simon Ezekiel Odunga
  4. Kondoa           Sezeria Veneranda Makutta
  5. Bahi            Elizabeth Simon
  6. Mpwapwa            Jabir Mussa Shekimweli
  7. Kongwa            John Ernest Palingo
GEITA
  1. Bukombe            Josephat Maganga
  2. Mbogwe            Matha John Mkupasi
  3. Nyang�wale            Hamim Buzohera Gwiyama
  4. Geita            Herman C. Kipufi
  5. Chato            Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
  1. Mufindi        Jamhuri David William
  2. Kilolo            Asia Juma Abdallah
  3. Iringa            Richard Kasesela
KAGERA
  1. Biharamulo            Saada Abraham Mallunde
  2. Karagwe            Geofrey Muheluka Ayoub
  3. Muleba            Richard Henry Ruyango
  4. Kyerwa            Shaban Ilangu Lissu
  5. Bukoba            Deodatus Lucas Kinawilo
  6. Ngara            Col. Michael M. Mtenjele
  7. Missenyi            Col Denis F. Mwila
KATAVI
  1. Mlele            Rachiel Stephano Kasanda
  2. Mpanda            Lilian Charles Matinga
  3. Tanganyika            Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
  1. Kigoma            Samsoni Renard Anga
  2. Kasulu                        Martin Elia Mkisi
  3. Kakonko            Hosea Malonda Ndagala
  4. Uvinza                        Mwanamvua Hoza Mlindoko
  5. Buhigwe            Elisha Marco Gagisti
  6. Kibondo            Luis Peter Bura
KILIMANJARO
  1. Siha            Onesmo Buswelu
  2. Moshi        Kippi Warioba
  3. Mwanga     Aaron Yeseya Mmbago
  4. Rombo       Fatma Hassan Toufiq
  5. Hai            Gelasius Byakanwa
  6. Same        Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
  1. Nachingwea           Rukia Akhibu Muwango
  2. Ruangwa            Joseph Joseph Mkirikiti
  3. Liwale            Sarah Vicent Chiwamba
  4. Lindi            Shaibu Issa Ndemanga
  5. Kilwa            Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
  1. Babati            Raymond H. Mushi
  2. Mbulu            Chelestion Simba M. Mofungu
  3. Hanang�            Sara Msafiri Ally
  4. Kiteto            Tumaini Benson Magessa
  5. Simanjiro            Zephania Adriano Chaula
MARA
  1. Rorya            Simon K. Chacha
  2. Serengeti            Emile Yotham Ntakamulenga
  3. Bunda            Lydia Simeon Bupilipili
  4. Butiama            Anarose Nyamubi
  5. Tarime            Glodious Benard Luoga
  6. Musoma            Vicent Anney Naano
MBEYA
  1. Chunya            Rehema Manase Madusa
  2. Kyela            Claudia Undalusyege Kitta
  3. Mbeya           William Ntinika Paul
  4. Rungwe            Chalya Julius Nyangidu
  5. Mbarali            Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
  1. Gairo            Siriel Shaid Mchembe
  2. Kilombero            James Mugendi Ihunyo
  3. Mvomero            Mohamed Mussa Utali
  4. Morogoro            Regina Reginald Chonjo
  5. Ulanga                        Kassema Jacob Joseph
  6. Kilosa            Adam Idd Mgoyi
  7. Malinyi            Majula Mateko Kasika
MTWARA
  1. Newala            Aziza Ally Mangosongo
  2. Nanyumbu            Joakim Wangabo
  3. Mtwara            Khatibu Malimi Kazungu
  4. Masasi            Seleman Mzee Seleman
  5. Tandahimba            Sebastian M. Walyuba
MWANZA
  1. Ilemela            Leonald Moses Massale
  2. Kwimba            Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
  3. Sengerema            Emmanuel Enock Kipole
  4. Nyamagana            Mary Tesha Onesmo
  5. Magu            Hadija Rashid Nyembo
  6. Ukerewe            Estomihn Fransis Chang�ah
  7. Misungwi            Juma Sweda
NJOMBE
  1. Njombe            Ruth Blasio Msafiri
  2. Ludewa                        Andrea Axwesso Tsere
  3. Wanging�ombe            Ally Mohamed Kassige
  4. Makete                        Veronica Kessy
PWANI
  1. Bagamoyo            Alhaji Majid Hemed Mwanga
  2. Mkuranga            Filberto H. Sanga
  3. Rufiji            Juma Abdallah Njwayo
  4. Mafia            Shaibu Ahamed Nunduma
  5. Kibaha            Asumpter Nsunju Mshama
  6. Kisarawe            Happyness Seneda William
  7. Kibiti            Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
  1. Sumbawanga            Khalfan Boniface Haule
  2. Nkasi            Said Mohamed Mtanda
  3. Kalambo            Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
  1. Namtumbo            Luckness Adrian Amlima
  2. Mbinga            Cosmas Nyano Nshenye
  3. Nyasa            Isabera Octava Chilumba
  4. Tunduru            Juma Homela
  5. Songea            Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
  1. Kishapu            Nyambonga Daudi Taraba
  2. Kahama            Fadhili Nkulu
  3. Shinyanga            Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
  1. Busega            Tano Seif Mwera
  2. Maswa            Sefu Abdallah Shekalaghe
  3. Bariadi            Festo Sheimu Kiswaga
  4. Meatu            Joseph Elieza Chilongani
  5. Itilima            Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
  1. Mkalama            Jackson Jonas Masako
  2. Manyoni            Mwembe Idephonce Geofrey
  3. Singida            Elias Choro John Tarimo
  4. Ikungi            Fikiri Avias Said
  5. Iramba            Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
  1. Songwe            Samwel Jeremiah
  2. Ileje            Joseph Modest Mkude
  3. Mbozi            Ally Masoud Maswanya
  4. Momba            Juma Said Irando
TABORA
  1. Nzega            Geofrey William Ngudula
  2. Kaliua            Busalama Abel Yeji
  3. Igunga            Mwaipopo John Gabriel
  4. Sikonge            Peres Boniphace Magiri
  5. Tabora            Queen Mwashinga Mlozi
  6. Urambo            Angelina John Kwingwa
  7. Uyui            Gabriel Simon Mnyele
TANGA
  1. Tanga            Thobias Mwilapwa
  2. Muheza            Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
  3. Mkinga            Yona Lucas Maki
  4. Pangani            Zainab Abdallah Issa
  5. Handeni            Godwin Crydon Gondwe
  6. Korogwe            Robert Gabriel
  7. Kilindi            Sauda Salum Mtondoo
  8. Lushoto            Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016
Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya, June 26 2016 huu hapa Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya, June 26 2016 huu hapa Reviewed by ISSAH JUMA on Sunday, June 26, 2016 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.