Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
- Arusha Mrisho Mashaka Gambo
- Arumeru Alexander Pastory Mnyeti
- Ngorongoro Rashid Mfaume Taka
- Longido Daniel Geofrey Chongolo
- Monduli Idd Hassan Kimanta
- Karatu Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
- Kinondoni Ally Hapi
- Ilala Sophia Mjema
- Temeke Felix Jackson Lyaviva
- Kigamboni Hashim Shaibu Mgandilwa
- Ubungo Hamphrey Polepole
DODOMA
- Chamwino Vumilia Justine Nyamoga
- Dodoma Christina Solomon Mndeme
- Chemba Simon Ezekiel Odunga
- Kondoa Sezeria Veneranda Makutta
- Bahi Elizabeth Simon
- Mpwapwa Jabir Mussa Shekimweli
- Kongwa John Ernest Palingo
GEITA
- Bukombe Josephat Maganga
- Mbogwe Matha John Mkupasi
- Nyang�wale Hamim Buzohera Gwiyama
- Geita Herman C. Kipufi
- Chato Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
- Mufindi Jamhuri David William
- Kilolo Asia Juma Abdallah
- Iringa Richard Kasesela
KAGERA
- Biharamulo Saada Abraham Mallunde
- Karagwe Geofrey Muheluka Ayoub
- Muleba Richard Henry Ruyango
- Kyerwa Shaban Ilangu Lissu
- Bukoba Deodatus Lucas Kinawilo
- Ngara Col. Michael M. Mtenjele
- Missenyi Col Denis F. Mwila
KATAVI
- Mlele Rachiel Stephano Kasanda
- Mpanda Lilian Charles Matinga
- Tanganyika Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
- Kigoma Samsoni Renard Anga
- Kasulu Martin Elia Mkisi
- Kakonko Hosea Malonda Ndagala
- Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko
- Buhigwe Elisha Marco Gagisti
- Kibondo Luis Peter Bura
KILIMANJARO
- Siha Onesmo Buswelu
- Moshi Kippi Warioba
- Mwanga Aaron Yeseya Mmbago
- Rombo Fatma Hassan Toufiq
- Hai Gelasius Byakanwa
- Same Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
- Nachingwea Rukia Akhibu Muwango
- Ruangwa Joseph Joseph Mkirikiti
- Liwale Sarah Vicent Chiwamba
- Lindi Shaibu Issa Ndemanga
- Kilwa Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
- Babati Raymond H. Mushi
- Mbulu Chelestion Simba M. Mofungu
- Hanang� Sara Msafiri Ally
- Kiteto Tumaini Benson Magessa
- Simanjiro Zephania Adriano Chaula
MARA
- Rorya Simon K. Chacha
- Serengeti Emile Yotham Ntakamulenga
- Bunda Lydia Simeon Bupilipili
- Butiama Anarose Nyamubi
- Tarime Glodious Benard Luoga
- Musoma Vicent Anney Naano
MBEYA
- Chunya Rehema Manase Madusa
- Kyela Claudia Undalusyege Kitta
- Mbeya William Ntinika Paul
- Rungwe Chalya Julius Nyangidu
- Mbarali Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
- Gairo Siriel Shaid Mchembe
- Kilombero James Mugendi Ihunyo
- Mvomero Mohamed Mussa Utali
- Morogoro Regina Reginald Chonjo
- Ulanga Kassema Jacob Joseph
- Kilosa Adam Idd Mgoyi
- Malinyi Majula Mateko Kasika
MTWARA
- Newala Aziza Ally Mangosongo
- Nanyumbu Joakim Wangabo
- Mtwara Khatibu Malimi Kazungu
- Masasi Seleman Mzee Seleman
- Tandahimba Sebastian M. Walyuba
MWANZA
- Ilemela Leonald Moses Massale
- Kwimba Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
- Sengerema Emmanuel Enock Kipole
- Nyamagana Mary Tesha Onesmo
- Magu Hadija Rashid Nyembo
- Ukerewe Estomihn Fransis Chang�ah
- Misungwi Juma Sweda
NJOMBE
- Njombe Ruth Blasio Msafiri
- Ludewa Andrea Axwesso Tsere
- Wanging�ombe Ally Mohamed Kassige
- Makete Veronica Kessy
PWANI
- Bagamoyo Alhaji Majid Hemed Mwanga
- Mkuranga Filberto H. Sanga
- Rufiji Juma Abdallah Njwayo
- Mafia Shaibu Ahamed Nunduma
- Kibaha Asumpter Nsunju Mshama
- Kisarawe Happyness Seneda William
- Kibiti Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
- Sumbawanga Khalfan Boniface Haule
- Nkasi Said Mohamed Mtanda
- Kalambo Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
- Namtumbo Luckness Adrian Amlima
- Mbinga Cosmas Nyano Nshenye
- Nyasa Isabera Octava Chilumba
- Tunduru Juma Homela
- Songea Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
- Kishapu Nyambonga Daudi Taraba
- Kahama Fadhili Nkulu
- Shinyanga Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
- Busega Tano Seif Mwera
- Maswa Sefu Abdallah Shekalaghe
- Bariadi Festo Sheimu Kiswaga
- Meatu Joseph Elieza Chilongani
- Itilima Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
- Mkalama Jackson Jonas Masako
- Manyoni Mwembe Idephonce Geofrey
- Singida Elias Choro John Tarimo
- Ikungi Fikiri Avias Said
- Iramba Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
- Songwe Samwel Jeremiah
- Ileje Joseph Modest Mkude
- Mbozi Ally Masoud Maswanya
- Momba Juma Said Irando
TABORA
- Nzega Geofrey William Ngudula
- Kaliua Busalama Abel Yeji
- Igunga Mwaipopo John Gabriel
- Sikonge Peres Boniphace Magiri
- Tabora Queen Mwashinga Mlozi
- Urambo Angelina John Kwingwa
- Uyui Gabriel Simon Mnyele
TANGA
- Tanga Thobias Mwilapwa
- Muheza Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
- Mkinga Yona Lucas Maki
- Pangani Zainab Abdallah Issa
- Handeni Godwin Crydon Gondwe
- Korogwe Robert Gabriel
- Kilindi Sauda Salum Mtondoo
- Lushoto Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016
Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya, June 26 2016 huu hapa
Reviewed by ISSAH JUMA
on
Sunday, June 26, 2016
Rating:
No comments: