Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D - (x 15) at Tume ya Utumishi wa Mahakama

Application Deadline: 16 Feb 2015
Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D - (x 15) POSITION DESCRIPTION:

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa mujibu wa aya ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

Hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia watanzania wenye sifa zilizo ainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wapo tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania ambazo zipo katika mikoa na wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.


Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D - Nafasi 15.
Sifa
Shahada/Stashahada ya Juu katika masomo ya Sayansi ya Kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinacho tambuliwa na Serikali.

Waombaji watapangiwa kazi Mahakama Kuu - Kanda isipokuwa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe kanda tatu (3) kati ya zifuatazo: Arusha, Bukoba, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mwanza, Mtwara, Songea, Sumbawanga, Tabora na Tanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza lisizingatiwe.
5.3 Kazi za Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja II
(i) Kuweka kumbukumbu za taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi.
(ii) Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na udhibiti unaohusu Kompyuta.
(iii) Kutoa msaada wa kiufundi kwa Wizara/Idara/Vituo mbalimbali vya kazi.

APPLICATION INSTRUCTIONS:
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV)
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Waombaji walio katika utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa Umma waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa Umma.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P 8391, DAR ES SALAAM.

Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015 saa 9:30 Alasiri.
Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D - (x 15) at Tume ya Utumishi wa Mahakama Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D - (x 15) at Tume ya Utumishi wa Mahakama Reviewed by ISSAH JUMA on Monday, February 09, 2015 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.