Mtendaji Wa Mtaa III- x 73 Halmashauri ya Mji wa Bariadi

Application Deadline: 12 Oct 2015
Mtendaji Wa Mtaa III- x 73 POSITION DESCRIPTION:
From Mwananchi, 21st Septemba2015

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi anatangaza nafasi za kazi themanini na moja (81). Maombi ya kujaza nafasi tajwa hapa chini yanakaribishwa kutoka kwa Mtanzania yeyote mwenye sifa ·zilizotajwa katika tangazo hili.

Nafasi zinazotangazwa 'ni kama ifuatavyo:-

MTENDAJI WA MTAA ill: Nafasi 73
Ngazi ya Mshahara: TGS B
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
Awe amehitimu Elimu ya Kidato Cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahadal
cheti katika'moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo
ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na serikali.

Majukumu:
(i) Kuratibu na kutekeleza Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri
(ii) Kuishauri kamati ya Maendeleo ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katikaMtaa.
(iii) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo na sheria zingine zinazoturnika katika Mtaa.
(iv) Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
(v) Kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo katika Mtaa.
(vi) Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.


Sifa nyingine za Jumla:
(i) Mwombaji awe raia wa Tanzania
(ii) Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 40.
(iii} Maombi yake yaambatishwe picha (passport size) na vielelezo rya sifa zake.
(iv) Cheti cha kuzaliwa kiambatishwe pia
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi,
Halmashauri ya Mji
S.L.P. 526, Bariadi
Tangazo hili Iimetolewa leo tarehe 21.09.2015


Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12.10.2015 saa tisa na nusu (9:30) Alasiri
Mtendaji Wa Mtaa III- x 73 Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mtendaji Wa Mtaa III- x 73 Halmashauri ya Mji wa Bariadi Reviewed by ISSAH JUMA on Monday, September 21, 2015 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.