Mhasibu Mkuu-(x2) at Boimanda Modern Construction Co Ltd

Application Deadline: 31-12-2016

Description
From Guardian, 2nd Dec 2016

BOIMANDA MODERN CONSTRUCTION CO LTD

INATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZIFUATAZO

Mhasibu Mkuu (Nafasi mbili)
a. Sifa

Awe tayari kufanya kazi katika mkoa wa Iringa , Njombe au katika kituo chochote atakachopangiwa na mwajiri.
Awe na shahada katika masomo ya uhasibu kutoka katika chuo chochote kinachotambuliwa na amesajiliwa na
mamlaka za kisheria
Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu, kanuni na sheria za makampuni
Awe na uzoefu ama uelewa wa kinadharia wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kornpyuta (Accounting packages)
Awe mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe
Awe na uzoefu wa kazi hii wa kipindi kisichopungua miaka miwili
Awe na umrl wa kati ya miaka 25 na 45

b. Majukumu
Ndiye atakayehidhinisha hati za malipo kwa maelekezo na kwa kuzingatia taratibu za kampuni
Ataandaa taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi
.Ataslmamta wahasibu wasaidizi katika kazi zao za kila siku
Atasimamia shughuli za uhasibu kwenye kitengo cha Idara
Ataandika taarifa ya maduhuli
Kutayarisha ripoti maalumu ya fedha kwa kukusanya, kuchambua na kufupisha maelezo ya akaunti
Awe na uwezo wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA
Atahakikisha malipo kwa wafanyakazi na vyama vingine yanafanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa
kufuata miongozo na sera ya kampuni
Atachambua mwenendo wa mapato na matumizi ya kampuni na kupendekeza viwango vya bajeti vinavyokwenda
sambamba na udhibiti wa matumizi
Kufanya kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti

Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.
Mhasibu Mkuu-(x2) at Boimanda Modern Construction Co Ltd Mhasibu Mkuu-(x2) at Boimanda Modern Construction Co Ltd Reviewed by ISSAH JUMA on Thursday, December 08, 2016 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.