Katibu Mahsusi Daraja La III X 5 Manispaa ya Kinondoni

Application deadline 2017-08-14
Location
Dar Es Salaam
Description
Mwananchi 1/8/2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni anapenda kuwatangaiia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo :-
SIFA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na
kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya
Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata
mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali
na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet,
E-mail na Publisher.

KAZI NA MAJUKUMU.
Katibu Mahsusi Dar-aja la III atapagiwa kufanya kazi katika "Typing Pool" au
chini ya Katibu Mahsusi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye
ofisi ya Mkuu wa sehemu au kitengo.
i) Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
ii) Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza
sehemu wanapoweza kushughulikiwa
iii) Kusaidia kutunza taarifa aukumbukumbu za matukio, miadi, wageni,
tarehe za vikao safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu
Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
iv) Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu
chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v) Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi
wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa
na wasaidizi hao.
vi) Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika
sehemu alipo,na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu
zinazohusika.
vii) Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake
wa kazi.

NGAZI VA M5HAHARA - TG5. B
MASHARTI YA JUMLA:
Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania.
Awe amehitimu na Kupata Cheti cha Taaluma cha Kidato cha Nne (IV) au (VI) NB. Results Slip hazikubaliki
Awe na Cheti cha Kuzaliwa
Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo;-
i) Nakala za Vyeti vya Mwombaji vilivyothibitishwa.
ii) Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae).
iii) Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji
za hivi karibuni.
Kila mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka 18 - 45
Waombaji wenye Sifa Pungufu au zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauri kuomba.

APPLICATION
Barua zote za maombi ziandikwe kwa rnkono, zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA VA KINONOONI
S. L. P. 31902
2BARABARA YA MOROGORO,
14883 DAR ES SALAAM.
Katibu Mahsusi Daraja La III X 5 Manispaa ya Kinondoni Katibu Mahsusi Daraja La III X 5 Manispaa ya Kinondoni Reviewed by ISSAH JUMA on Wednesday, August 09, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.