DEREVA – (30 NAFASI )


Job Description

DEREVA – (30 NAFASI )
1.1MAJUKUMU YA KAZI
i.Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii.Kuwapeleka watumishi katika maeneo mbalimbali ya kikazi;
iii.Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
iv.Kusafirisha mizigo na nyaraka mbalimbali za ofisi;
v.Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
vi.Kufanya usafi wa gari na;
vii.Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI:
Mwombaji awe na cheti cha kufaulu cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, Waombaji ambao wamewahi kufanya kazi za kuendesha magari katika kufanya tafiti mbalimbali watafikiriwa kwanza.
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote watambue kuwa Kituo cha kazi ni Dodoma. Pamoja na hilo NBS haitahusika na gharama za kuhudhuria usaili na kuripoti kazini kwa wale watakaofaulu usaili na kuchaguliwa;
iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa;
iv. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo;
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika;
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
– Taarifa ya Polisi ya kutokuwa na ajili (Police Traffic clearance Report).
vii. Hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 Julai, 2018.
xiii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI
ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU.
ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA
KATIBU,
OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 63100
DAR ES SALAAM 
DEREVA – (30 NAFASI ) DEREVA – (30 NAFASI ) Reviewed by ISSAH JUMA on Tuesday, July 31, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.