KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III, - 21 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2020-01-04
Application Deadline: 2020-01-18


JOB SUMMARY:
NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
·         Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
·         Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
·         Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
·         Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
·         Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
·         Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
·         Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
·         Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.  Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
REMUNERATION: Salary Scale TGS. B
Login to Apply
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III, - 21 POST KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III, - 21 POST Reviewed by ISSAH JUMA on Sunday, January 05, 2020 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.