Katibu Muhtasi III - (x2) Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

Application Deadline: 29 Jul 2015
Katibu Muhtasi III - (x2) POSITION DESCRIPTION:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa anawatangazia wananchi wote wenye sifa zinazotakiwa kuomba
kujaza nafasi za kazi mbalimbali kama ifuatavyo:-

KATIBU MUHTASIIII - (NAFASI 2)

SIFA/ELIMU/UJUZI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ra Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya
Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na
wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikall na kupa'ta
cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

KAZI NA MAJUKUMU
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza
kushughulikiwa.
Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu
wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumuarifu
Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika
katika shughuli za kazi hapo ofisini. .
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu
taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya,
kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
UMRI- Mwombaji awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40.

MSHAHARA
Kianzio cha ngazi ya mshahara ni TGS. B (1).
APPLICATION INSTRUCTIONS:
MAELEZO YA JUMLA
Maombi yote yawasilishwe yakiwa yameambatishwa na CV pamoja na nakala za vyeti vya kuhitimu elimu na mafunzo {vyeti vinavyoonyesha kiwango cha kufaulu sio "Leaving Certificate

MUHIMU
MUOMBAJI ANATAKIWA KUTUMIA VYETI VYAKE HALISI NA HALALI, KWANI UHAKIKI WA VYETI UTAFANYIKA BARAZA
LA MITIHANI NA VYUO VYA MAFUNZO ALIVYOPITIA. ENDAPO ITAJULIKANA KUWA NA UDANGANYIFU WA AINA
YOYOTE HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA.
WAOMBAJI WALIOHITIMU MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA WATAPEWA KIPAUMBELE KWA KUWA MAFUNZO
HAYO NI MUHIMU YENYE KULETA UZALENDO NA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.
Maombi yatumwe kwa Anwani ifuatayo:-
MKURUGENZI MTENDAJI WllAYA
HALMASHAURI VA WILAVA VA KILOSA
S.L.P 65
KILOSA
Mwisho wa kupokea maombi ni siku kumi na nne (14) baada ya kutolewa Tangazo.
Imetolewa na:
Idd A. Mshili
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA VA KILOSA
Katibu Muhtasi III - (x2) Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Katibu Muhtasi III - (x2) Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Reviewed by ISSAH JUMA on Thursday, July 16, 2015 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.